Friday, December 7, 2012

WADAU TUNAOMBA MICHANGO YENU-HII NI SADAKA

Wakazi hawa wa Mtaa wa Kingugi,wanauchungu na kuharibika kwa mazingira ya Mtaa wao wapo bega kwa bega katika kujitolea katika ujenzi wa Mtaro ili kupunguza kasi ya maji  ambayo inaleta uharibifu.Utaratibu huu wa kujitolea umeanza rasmi tarehe 1/12/2012 na niendelevu.
Baada ya kusambaza Serela mbili za mawe, Wakazi hawa wanasubiri Serela jingine kutoka Mji mwema.
 
Hii ni hali halisi,tunahitaji misaada ya hali na mali ili tuweze kuokoa mazingira ya Mtaa wa Kingugi.Kuna usemi usemao "Binaadamu hashindwi na mazingira yake".Kwa hiyo Wakazi wa Kingugi,Marafiki,Mashirika ya kitaifa na Kimataifa, taasisi mbali mbali,Wasomi,Wanasiasa na watu wote wanaopenda maendeleo tunaomba michango yenu ya hali na mali.

No comments:

Post a Comment