Hii ni hali halisi,tunahitaji misaada ya hali na mali ili tuweze kuokoa mazingira ya Mtaa wa Kingugi.Kuna usemi usemao "Binaadamu hashindwi na mazingira yake".Kwa hiyo Wakazi wa Kingugi,Marafiki,Mashirika ya kitaifa na Kimataifa, taasisi mbali mbali,Wasomi,Wanasiasa na watu wote wanaopenda maendeleo tunaomba michango yenu ya hali na mali.
Friday, December 7, 2012
WADAU TUNAOMBA MICHANGO YENU-HII NI SADAKA
Wakazi hawa wa Mtaa wa Kingugi,wanauchungu na kuharibika kwa mazingira ya Mtaa wao wapo bega kwa bega katika kujitolea katika ujenzi wa Mtaro ili kupunguza kasi ya maji ambayo inaleta uharibifu.Utaratibu huu wa kujitolea umeanza rasmi tarehe 1/12/2012 na niendelevu.
Baada ya kusambaza Serela mbili za mawe, Wakazi hawa wanasubiri Serela jingine kutoka Mji mwema.
KULINDA MAZINGIRA YA MTAA WA KINGUGI
Baadhi ya Wakazi wa Mtaa wa Kingugi Kata ya Kiburugwa wa kijitolea kwa nguvu na mali katika kuboresha mazingira ya Mtaa wao chini ya Mhandisi wa Mtaa Ndugu Siraji Rajabu.Hii ilikuwa siku ya Jumapili ya tarehe 2/12/2012.
Mvua zilizonyesha mwishoni mwa mwezi wa Novemba,2012 zilileta athari kama inavyoonekana katika picha.Hili ni eneo la msikiti wa kwa Dumba lume.Mhe. Diwani Mawazo Waziri wa Kata ya Kiburugwa akisisitiza jambo kuhusu miundo mbinu katika mkutano wa hadhara Mtaa wa Kingugi mapema Novemba,2012.
Mkazi wa Kingugi,Yahya Dihenga akijitolea kujenga Mtaro kuelekea Mto Mzinga siku ya Jumapili, tarehe 2/12/2012.Huu ni utaratibu ambao Wakazi wa Kingugi wamejiwekea kila siku ya Jumapili lazima wafanye jambo fulani kuhusu mazingira yao.
Subscribe to:
Comments (Atom)